Jinsi IR Remotes Zinavofanya Kazi
Kila siku tunanyakua remote, tunapress button, TV inawaka. Tunabadilisha channel, volume, na mengine yote. Lakini je, umewahi relax na kujiuliza - hii kitu inafanyaje kazi bila waya wowote? Leo tutazama kwa undani kuhusi teknolojia hii.
HISTORIA KIDOGO - REMOTE ZA ZAMANI
Kwanza kabisa, wacha tujue remote control haikuanza na TV! Miaka ya 1950s, watu walikuwa wanachoka kuamka kila mara kubadilisha channel. TV za wakati huo zilikuwa na knobs za kugeuzwa. Imagine, lazima uamke kutoka kwa sofa yako ya starehe kila unapotaka kubadilisha channel!

Remote ya kwanza ilikuwa na waya! ndio, ulifunga waya kutoka kwa remote hadi kwa TV. Ilikuwa kama kubadilisha channel na kamba ndefu.
Kisha wakaja na "Flashmatic" mwaka 1955 - ilikuwa inatuma mwanga wa kawaida kwa TV! Shida? Ukifungua curtains na jua likaingia, TV ingeanza kubadilisha channels zenyewe! Chaos tupu!
INFRARED - MWANGA USIOONEKANA
Infrared ni aina ya mwanga ambao ni invisible kwa macho ya binadamu. Kuna types nyingi za mwanga - visible light (tunaouona), UV rays (za jua zinazotuchoma), X-rays (za hospital), na infrared.

Infrared iko kati ya visible light na microwaves. Wavelength yake ni ndefu kuliko red light, ndiyo maana tunaiita "infra-red" - yaani chini ya nyekundu.
Fun fact: Vitu vyote vya moto hutoa infrared! Hata wewe sasa hivi unatoa infrared waves. Ndiyo maana night vision goggles zinafanya kazi - zinaona heat yako kama infrared!
Remote Inafanyaje Kazi?
Hebu fikiria hivi - unapobonyeza button ya volume au channel, remote inafanya mambo matatu:
Kwanza, inachukua command yako. Kila button ina code yake - kama password. Button ya "power" ina code tofauti na ya "volume up".
Pili, inabadilisha hiyo code kuwa mwanga. LED ndogo ile nyekundu unaiona mwisho wa remote ndiyo inafanya kazi hii. Inawasha na kuzima kwa pattern fulani - pengine mara elfu kumi kwa sekunde! Kwa mfano, code ya "volume up" inaweza kuwa kitu kama: washa-zima-zima-washa-washa-zima... na kadhalika.
Tatu, TV yako ina sensor (kitu kama jicho) ambalo linaona huo mwanga wa infrared. Linapokea ile pattern na kuisoma kama message.

Je, Kwa Nini TV Hachanganyi Remote Ya DVD Na Yake?
Kila kampuni ina "lugha" yake. Sony wanaongea lugha tofauti na Samsung. Hata kama ni same brand, kila gadget ina address yake - kama namba ya simu. Remote ya TV yako inasema "TV ya Samsung namba 123, washa!" Hivyo DVD haitalisten kwa sababu si yake hiyo message.